Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeHabariRais wa China, ampongeza Dkt Samia amuahidi ushirikiano

Rais wa China, ampongeza Dkt Samia amuahidi ushirikiano

Rais wa China, Xi Jinping ametuma salamu za pongezi kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya kuibuka kidedea katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Dkt. Samia alipata ushindi wa kishindo wa kura milioni 31.913,866 sawa na asilimia 97.66 zilizomwezesha kuendelea kuwaongoza Watanzania kwa muhula mwingine wa miaka mitano.

Rais Xi Jinping anaungana na viongozi wa mataifa mbalimbali akiwemo Rais wa Urusi, Vladmir Putin ambaye jana alituma ujumbe maalumu wa pongezi uliokwenda kuonana na Dkt. Samia Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

Katika ujumbe wake wa jana Alhamisi Novemba 6,2025 Rais Xi Jinping anayeongoza Taifa lenye uchumi mkubwa duniani, amempongeza Dkt. Samia kwa kuapishwa ili kuongoza Tanzania kwa muhula mwingine.

“Nimefurahishwa kujua kuhusu kuanza kwako rasmi kwa majukumu ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nakupongeza kwa dhati kwa niaba ya Serikali na watu wa China”.
“Nakutakia kila mafanikio katika kutekeleza jukumu hili tukufu, na mafanikio makubwa zaidi katika kuwaongoza wananchi wa Tanzania kuelekea maendeleo ya taifa na ustawi mpya”, ameandika Rais Xi Jinping.

Katika ujumbe huo, Rais Xi Jinping amesema ana thamini kiwango cha juu cha maendeleo baina ya China na Tanzania, na kwamba atafanya kazi kwa ushirikiano na Rais Dkt. Samia ili kutekeleza matokeo ya Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika Beijing.

Mbali na hilo, kiongozi huyo ameelezea dhamira yake ya kuinua ushirikiano wa kimkakati na wa kina kati ya taifa hilo na Tanzania, ili kufikia ngazi ya juu ya kujenga jumuiya ya kudumu ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika enzi mpya.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments