Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amezua kicheko baada ya kutoa kauli ya utani wakati wa hafla iliyohudhuriwa na Waziri Mkuu.
Akizungumza mbele ya hadhira, Chalamila amesema kwa mzaha kuwa tangu asikie uvumi unaodai mtu akiguswa begani anaweza kupoteza sehemu zake za siri, amekuwa makini zaidi.
Ameongeza kwa utani kuwa hana mali nyingine ya thamani, hivyo hawezi kuruhusu “kuibiwa” kwa namna hiyo, kauli iliyowafanya wengi kucheka huku ikigusa pia mjadala unaoendelea kuhusu imani potofu zinazosambaa katika jamii.




