Wednesday, April 1, 2026
spot_img
HomeHabariRC Malisa akabidhi boti kuimarisha ulinzi Ziwa Nyasa

RC Malisa akabidhi boti kuimarisha ulinzi Ziwa Nyasa

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Beno Malisa amemkabidhi boti moja mpya PB.44 ya Ulinzi kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga.

Malisa amekabidhi boti hiyo, Agosti 22,2025 na kulitaka  Jeshi la Polisi mkoani humo kuitumia vizuri  kwenye shughuli za kuimarisha doria za ziwa nyasa lililopo wilayani Kyela ili  na kutokomeza uhalifu.

“Boti hii ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura kuimarisha ulinzi ziwa Nyasa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga amesema kupitia boti hiyo watafanya doria na kuimarisha  ulinzi ndani ya ziwa hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, Jeshi la Wananchi JWTZ, Uhamiaji na Mamlaka ya Mapato TRA.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments