Wednesday, December 17, 2025
spot_img
HomeHabariREA yashinda tuzo utoaji huduma kwenye utumishi wa umma 

REA yashinda tuzo utoaji huduma kwenye utumishi wa umma 

📌Ni tuzo ya ubora katika kushughulikia malalamiko kwa Wananchi na kutoa mrejesho

📌Vigezo vyav usambazaji wa umeme kwenye vijiji vyote; vitongoji zaidi elfu 30 pamoja na usambazaji wa nishati safi, vimechangia

Dar es Salaam📍

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeshinda tuzo ya Taasisi Bora inayoshughulikia malalamiko ya Wateja pamoja na kutoa mrejesho kwa wakati katika utoaji wa huduma kwa umma (Watanzania) kwa mwaka 2025.

Tuzo hiyo imetolewa usiku wa tarehe 16 Desemba, 2025 na Bwana, Shariff Shariff; Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Uwekezaji kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kupokelewa na Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, Mhandisi, Jones Olotu kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa REA katika ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.

Hafla ya utoaji wa tuzo hizo, imeandaliwa na Taasisi ya Tanzania Professional Skills and Innovation Awards (TPSIA) kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wa maendeleo na sekta binafsi ili kutambua na kuthamini mchango na jitihada za Taasisi za Umma kwa maendeleo ya Taifa.

Tuzo hizo zimepewa jina la Tuzo za Ubunifu kwenye Utumishi wa Umma (Public Service and Innovation Awards) ambapo zaidi ya Taasisi 300 za Serikali zimeshindanishwa katika makundi 29 ambapo REA imekuwa mshindi katika Kundi la 28 la Taasisi Bora iliyoshughulikia Malalamiko ya Wateja katika Utoaji wa Huduma kwa Umma mwaka 2025 hususan huduma za nishati vijijini (Customer Feedback and Complain Handling Award, 2025).

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mhandisi Olotu amesema, imekuja katika wakati sahihi ambao Wakala imekamilisha jukumu la kusambaza umeme kwenye vijiji vyote Tanzania Bara (Vijiji 12,318); umeme umesambazwa kwenye jumla ya vitongoji 39,003 kati ya vitongoji vyote 64,359 pamoja na kusambaza teknolojia za nishati safi ya kupikia kwa Watanzania ambapo zaidi ya mitungi ya gesi ya kupikia (LPG) laki nane (800,000) kwa bei ya ruzuku (Nusu Bei).

“Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu na Menejimenti ya REA; tunawashukuru Waandaaji wa tuzo hizi kwa kutambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na REA katika kusambaza nishati bora vijijini, tuzo hii imekuja katika kipindi fasaha, ambapo tumefikisha umeme kwenye vijiji vyote 12,318; tumefikisha umeme kwenye vitongoji 39,003 kati ya vitongoji vyote 64,359, kipindi ambacho tumehamasisha na kusambaza nishati safi ya kupikia, ambapo zaidi ya mitungi ya gesi laki nane (800,000) imesambazwa kwenye wilaya zote 139 za Tanzania Bara, tumefanya hivyo kwa kuwa, tunaamini umeme ni kichecheo kikubwa kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Wananchi wa vijijini.” Amekaririwa, Mhandisi, Olotu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments