Rotary Club yatoa msaada kwa Watoto wenye Ulemavu


Rais wa Klabu ya Rotary Masaki, Reshma Shah, amekabidhi vifaa vya mchezo wa tenisi na nguo za michezo kwa watoto 45 wenye ulemavu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mbio za hisani za baiskeli zitakazofanyika Agosti 8 jijini Dar es Salaam.

Shah amesema mbio hizo zitashirikisha waendesha baiskeli 300, na fedha zitakazopatikana zitaelekezwa kusaidia wanawake wanaofanya biashara ndogondogo.

Amesisitiza umuhimu wa kuwahusisha watoto wenye ulemavu katika michezo na kuwashauri wazazi kuwaruhusu kushiriki badala ya kuwafungia majumbani. Washindi wa mbio hizo watapata makombe na medali.

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya tenisi, Salum Mvita, amewashukuru wadhamini kwa kutambua mchango wa wachezaji wenye ulemavu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *