Samatta amshawishi nyota mpya Simba

Kiungo mshambuliaji mpya wa Simba, Morice Abraham, amesema kujiunga kwake na Wekundu wa Msimbazi kumefanikishwa na ushauri wa Mbwana Samatta, aliyewahi kuichezea timu hiyo 2010–2011.

Morice, aliyekuwa akicheza Serbia, amesema Samatta ndiye aliyemhimiza kusaini mkataba na Simba na amekuwa mshauri wake tangu 2020.

Mchezaji mwingine mpya wa Simba, Mkenya Mohamed Bajaber, amesema hakulala usingizi baada ya kupata taarifa ya kutakiwa na Simba, akieleza heshima ya kuichezea klabu kubwa inayofahamika Afrika nzima.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *