Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dk. Samia Suluhu Hassan, ameendelea na kampeni zake za Uchaguzi Mkuu ambapo leo, Septemba 18, 2025, ameshiriki katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Hamburu, Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar.
Katika mkutano huo, Dkt. Samia alionekana akishiriki katika matukio mbalimbali ya picha sambamba na viongozi na wananchi waliojitokeza kwa wingi kumuunga mkono. Tukio hilo limeonesha mwendelezo wa hamasa ya kampeni za CCM kuelekea uchaguzi mkuu ujao.










