Sanane Shenye anautaka ubunge Bariadi kwa tiketi ya ACT-Wazalendo

 Mwanachama wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ndugu Sanane Selena Shenye, leo amechukua fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Bariadi, mkoani Simiyu. Fomu hiyo imekabidhiwa rasmi na Katibu wa Jimbo, Ndugu Simoni John, katika ofisi za chama zilizopo Bariadi.

Sanane Shenye ni mzaliwa wa Meatu, mkoa wa Simiyu, na ana uzoefu mpana katika sekta ya elimu, uongozi wa kijamii pamoja na usimamizi wa biashara. Kwa sasa, anahudumu kama Meneja Mkuu wa Kampuni ya Bugali Investment Limited.

Katika maisha yake ya uongozi, Sanane aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Gitoya Malambo, Bariadi, kati ya mwaka 2019 hadi 2023. Aidha, amewahi kufanya kazi kama Mwalimu Mkuu Msaidizi na Mkuu wa Taaluma katika shule mbalimbali za sekondari. Kati ya mwaka 2014 hadi 2018, alikuwa Katibu wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) Mkoa wa Simiyu.

Kielimu, Sanane ni mhitimu wa masomo ya sayansi (PCM) katika Shule ya Sekondari ya Musoma Tech, na ana umahiri wa lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa kuzungumza na kuandika.

Kupitia hatua hii ya kuwania Ubunge, Sanane Shenye ameonesha dhamira thabiti ya kuwatumikia wananchi wa Bariadi kwa uadilifu, uwajibikaji na maono ya kuleta maendeleo ya kweli kwa jamii, kwa kutumia sera na misimamo ya ACT-Wazalendo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *