Sanga awataka wananchi wa Kaskazini kuthamini upendo kupunguza migogoro ya ardhi

KATIBU Mkuu Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anthony Sanga amewashauri wananchi wa Kanda ya Kaskazini kupendana kifamilia ili kupunguza changamoto ya migororo ya ardhi.

Sanga alitoa ushauri huo leo jijini Arusha alipokuwa katika banda la wizara hiyo lililopo kwenye wiki ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani, ambayo kitaifa inafanyika mkoani Arusha kesho, wakati akisikiliza kero za ardhi na kutoa huduma.

Amesema Mkoa wa Arusha na mikoa jirani wana changamoto nyingi za ardhi na maeneo mengi wamegundua inasababishwa na masuala ya kifamilia.

Aidha amesema ugomvi kati ya watoto na watoto au baina ya wazazi na watoto, pamoja na migawanyo ya urithi ni chanzo kikubwa cha kuzalisha migororo hiyo, hasa katika Kanda ya Kaskazini ambapo watu wengi huwabagua watoto wa kike katika urithi wa ardhi.

“lakini kikubwa tunachowasihi wananchi wapendane na kuvumiliana katika familia na kuwa wamoja,kugawa haki sawa za mirathi bila ubaguzi wa jinsia, tabia ya kugombana siyo nzuri tunashauri wajenge upendo hasa kama wanafamilia, kuanzia watoto na watoto na wazazi na mwisho wawe timu moja,”amesema.

Amekemea tabia ya baadhi ya watu kubagua watu na kuwanyima umiliki wa ardhi kwa kigezo cha ukabila, kwa kufanya hilo ni kwenda kinyume na shera za nchi.
Mwisho

“Tunakemea ardhi ya kabila fulani Tanzania hatuna hiyo, sisi serikali tunasema ardhi yote ya watanzania na Ssheria na sera zetu zinatambua hili. kwa hivyo tru yoyote anaruhusiwa na anaweza kukaa sehemu yoyote bila kujali hapo sio pa kabila lake,”amesema.

Pia ameshauri watu wote wanaoshindwa kesi zao mahakamani kuridhika au kufuata taratibunz akimahalama kama zinavyosema sababu wao hawana mamlka ya kuingilia maamuzi ya kimahakama.

“Ila hatuwezi kuwafukuza bali tunawasililiza na kuwashauri na pale tunapobaini huna haki tunawaambia na tunaomba ridhika usiendelee kuhangaika kutafuta wengine katika suala lako,”amesema

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *