Serikali imesema inaendelea kuimarisha uwezo wa ndani katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI kwa kutafuta vyanzo vya fedha vya ndani kupitia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI.
Akizungumza bungeni jijini Dodoma, Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba amesema hadi kufikia Februari 2026, Serikali imefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 26.8 kupitia mfuko huo.
Ameeleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuhakikisha nchi inajitegemea kifedha na kuimarisha uwezo wa ndani wa kugharimia mwitikio wa VVU na UKIMWI, hususan katika maeneo ya kinga, tiba na huduma kwa waathirika.
Dk. Nchemba alitoa kauli hiyo wakati akiwasilisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2026/2027.




