Serikali imewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kushangilia timu zote zinazoshiriki mashindano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), yanayoendelea Tanzania, Kenya na Uganda.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alisema haipendezi uwanja kuwa mtupu timu nyingine zisizo Taifa Stars zinapocheza.
Alieleza kuwa mashindano hayo yameleta faida za kiuchumi na kutangaza vivutio vya utalii nchini.
Msigwa aliipongeza Taifa Stars kwa kufuzu robo fainali wakiwa vinara wa Kundi B kwa pointi 9, na pia kuishukuru TFF na BMT kwa hamasa wanazotoa.
Vinara wa Kundi B watakutana na mshindi wa pili wa Kundi A, lenye Angola, DR Congo, Morocco, Zambia na Kenya, huku mechi hiyo ikipigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.


