Serikali yatambua mchango wa Amref Tanzania kusaidia NGOs

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Ali Khamis (kushoto), ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs Forum) 2025, amekabidhi cheti cha shukrani kwa Mkurugenzi Mkazi wa Amref Tanzania, ikiwa ni kutambua mchango wa shirika hilo katika kuwezesha ujenzi wa uwezo wa kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali ya ndani.

Hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma, Agosti 11, 2025, ikiwa ni sehemu ya kongamano la siku tatu (Agosti 11–13, 2025) linalolenga kuwaleta pamoja wadau wa sekta hiyo kubadilishana uzoefu, kuimarisha ushirikiano na kutathmini mchango wa mashirika hayo katika maendeleo ya Taifa kwa kipindi cha miaka mitano (2020–2025).

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *