Serikali yatoa rai ya maandalizi ya Jumuiya ya Madola

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango amelitaka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na sekta binafsi kushirikiana kuhakikisha Tanzania inafanya maandalizi madhubuti kwa ajili ya mashindano ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika Julai 23 hadi Agosti 3, 2026 huko Scotland.

Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa mapokezi ya Kifimbo cha Mfalme wa Uingereza kinachoashiria maandalizi ya mashindano hayo, Dk. Mpango alisisitiza umuhimu wa kushiriki kikamilifu na kupata medali nyingi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, alisema serikali imewekeza katika miundombinu na vipaji, na inajenga Kituo cha Michezo Babati, Manyara kutokana na hali ya hewa inayofanana na ya nchi zitakazoshiriki. Kituo hicho kitasaidia maandalizi ya timu za taifa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *