Sunday, October 12, 2025
spot_img
HomeHabariSHIMIWI ni mahala Pa kazi – Ziana Mlawa

SHIMIWI ni mahala Pa kazi – Ziana Mlawa

Asema Wizara ya Nishati ipambane irudi na ushindi

Asema Wizara ya Nishati iwe mfano kwa Wizara zingine

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Nishati,  Ziana Mlawa amesema kushiriki michezo mbali mbali inasaidia katika kujenga afya ya mwili na akili hivyo mtumishi anapopata nafasi ya kushiriki michezo yeyote aitumie ipasavyo pia husaidia hali itakayowajengea uwezo kujiamini zaidi ikiwemo katika maeneo ya kazi.

Mlawa ameyasema hayo alipokuwa akiwaaga watumishi wa Wizara ya Nishati watakao shiriki michezo ya SHIMIWI itakayofanyika jijini Mwanza kwanzia tarehe 1 Septemba 2025

” Pamoja na kushiriki michezo ambapo ni mbali na eneo la kazi mkumbuke mkiwa huko ni eneo la kazi nidhamu na uadilifu uwe kipau mbele mdaa wote muwapo kwenye michezo  hiyo.” amesisitiza Mlawa

Ameongeza kuwa watumishi hao wajitahidi wapate ushindi ambapo kwa ushindi huo Wizara itapata heshima njee na ndani ya Wizara.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments