Klabu za Simba na Yanga zimeteuliwa kushiriki mashindano ya CECAFA yatakayofanyika Septemba 2–15 jijini Dar es Salaam, kama maandalizi ya michuano ya CAF 2025/2026.

Mkurugenzi Mtendaji wa CECAFA, Auka Gecheo, amethibitisha kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na timu zimeombwa kuthibitisha ushiriki wao mapema.
Mbali na Simba, Yanga na Mlandege kutoka Tanzania, timu nyingine zilizotumwa barua za ushiriki ni Vipers SC (Uganda), El Merriekh SC (Sudan Kusini), Al Hilal (Sudan), Kenya Police FC (Kenya), Ethiopia Insurance (Ethiopia), MCC FC (Somalia), APR FC (Rwanda), Aigle Noir FC (Burundi), na ASAS Djibouti Telecom (Djibouti).
Kila kanda itatoa timu mbili zitakazoshiriki, na mashindano hayo yanatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.