Simba SC imetangaza mdhamini mpya Betway kwa mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Sh bilioni 20, ikiwa ni rekodi mpya ya udhamini mkubwa zaidi nchini.

Mkataba huu una thamani ya zaidi ya Sh bilioni 6.66 kwa mwaka, ukipiku ule wa zamani wa M-Bet (Sh bilioni 5.22 kwa mwaka) uliovunjika msimu uliopita.
Mjumbe wa Bodi ya Simba Salum Mhene ‘Try Again’ amesema fedha hizo zitaimarisha kikosi na usajili wa wachezaji wa kimataifa, huku TFF ikipongeza hatua hiyo.
Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuelekea Ismailia, Misri leo kwa kambi ya wiki mbili na mechi za kirafiki, na uongozi umetangaza kuanza kutaja majina ya usajili mpya kuanzia jana usiku.