Singida Black Stars imeuza kiungo wake Josephat Bada kwa JS Kablie ya Algeria, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa klabu kujiimarisha kisoka na kibiashara.

Aidha, wamesema wanaendelea na mazungumzo ya kuuza Sabri Kondo kwenda Sweden, huku pia wakizungumza na klabu ya Ismailia ya Misri kuhusu Marouf Tchakei.
Kwa upande mwingine, mshambuliaji nyota Jonathan Sowah, aliyefunga mabao 13 msimu uliopita, amejiunga rasmi na Simba SC, ikiwa ni sehemu ya makubaliano maalum kati ya klabu hizo.