Singida Black Stars imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Idrissa Diomande kutoka Zoman FC ya Ivory Coast, kuchukua nafasi ya Victorien Adebayor, ambaye ameondoka baada ya msimu mmoja.

Kocha Miguel Gamondi amependekeza mabadiliko hayo kuelekea msimu mpya ambapo Singida itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.
Mbali na Adebayor, wachezaji wengine walionyeshwa mlango wa kutokea ni Emmanuel Lobota na Habibu Kiyombo.
Singida pia imewasajili Andrew Simchimba kutoka Geita Gold na beki Kelvin Kijili kutoka Simba.
Msimu uliopita, Singida ilimaliza nafasi ya nne kwa pointi 57 na kufika fainali ya Kombe la FA, ikifungwa na Yanga.