Benki ya Stanbic Tanzania (@stanbicbanktz) imetoa zawadi za msimu wa sikukuu kupitia kampeni inayoendelea ya Masta wa Miamala.
Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyoambatana na semina kwa vijana kutoka taasisi mbalimbali, Mkuu wa kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Stanbic, Emmanuel Mahodanga alisema “Kampeni hii ya miezi mitatu inalenga kuongeza matumizi ya njia mbalimbali za malipo za benki ya Stanbic kuanzia kadi za Visa, ATM na mtandao smart App wenye zaidi ya mawakala 600, Internet banking na USSD 15029#”.
Aliongeza kusema huduma hii imebuniwa si tu kwa ajili ya kukuza matumizi ya kidigitali bali kuwahamasisha wateja wasiotumia akaunti zao ili kuwapatia nafasi kufurahia urahisi na usalama wa miamala isiyo na fedha taslimu.

Alihitisha kusema: “Tunaposherehekea miaka 30 nchini Tanzania, kampeni hii inaonyesha dhamira yetu ya kudumu ya kutembea na wateja wetu kwa kushiriki nao pamoja katika msimu huu wa sikukuu kwa kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo simu, friji, microwave na pesa taslimu.” Washindi walitoka taasisi mbalimbali zikiwemo GSM, TBL, BLUE COAST, KPMG na PWC.





