Straika Paul Peter atua JKT Tanzania

Mshambuliaji Paul Peter, aliyefunga mabao manane msimu uliopita akiwa na Dodoma Jiji, ametua JKT Tanzania kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu na mashindano mengine.

Taarifa ya klabu hiyo imesema imemsajili kutokana na uwezo wake mkubwa aliouonesha, na wana imani atasaidia kikosi hicho cha maafande.

Paul, aliyewahi pia kuichezea Azam FC, alikuwa mfungaji bora wa Dodoma Jiji msimu uliopita lakini alikataa kuongeza mkataba baada ya msimu kumalizika.

JKT Tanzania pia imetangaza kambi ya maandalizi jijini Arusha na kuachana na wachezaji saba akiwemo Mateo Antony na Ismail Aziz.

Ofisa Habari Masau Bwire amesema usajili unaoendelea unaashiria kuwa msimu mpya wa Ligi Kuu utakuwa na ushindani mkubwa zaidi ya uliopita.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *