Monday, February 9, 2026
spot_img
HomeHabariTaasisi zinazohudumia wananchi ziwasilishe taarifa zake baraza la madiwani-Kwagilwa

Taasisi zinazohudumia wananchi ziwasilishe taarifa zake baraza la madiwani-Kwagilwa

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Reuben Kwagilwa, ameelekeza taasisi za serikali zinazohudumia wananchi wilayani Handeni kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa majukumu yao katika Baraza la Madiwani ili kuongeza uwazi na kuwafanya wananchi kufahamu kazi zinazofanywa na serikali.

Akizungumza katika mkutano wa kupokea na kujadili taarifa za kata za Halmashauri ya Mji Handeni uliofanyika, Kwagilwa amesema ni muhimu kwa wakuu wa taasisi za serikali kuhudhuria vikao vya Baraza la Madiwani na kuwasilisha taarifa zao.

Amezitaja baadhi ya taasisi hizo kuwa ni pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mamlaka ya Maji pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), akisisitiza kuwa taasisi hizo zinawajibika moja kwa moja kwa wananchi.

Pamoja na hayo, amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni, Maryam Ukwaju, pamoja na wataalamu wa halmashauri hiyo kwa mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyopita na kuendelea kutekeleza ilani ya sasa.

Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Amiri Mwaliko, amempongeza Naibu Waziri Kwagilwa kwa kuaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika nafasi hiyo, akisema anaamini atatekeleza vyema majukumu yake katika kuisaidia TAMISEMI.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Salum Nyamwese ameahidi kuwapa ushirikiano Madiwani katika utekelezaji wa majukumu yao.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments