Tabora United yamfuata kiungo kutoka Cameroon

Klabu ya Tabora United ipo hatua za mwisho kumsajili kiungo mkabaji kutoka Cameroon, Palai Manjie, kuchukua nafasi ya Nelson Munganga anayejiunga na Dodoma Jiji.

Taarifa zinaeleza kuwa wawakilishi wa Manjie wapo Dar es Salaam kukamilisha dili hilo, huku kukiwa na wachezaji wengine wa kigeni walioko Ukonga kwa mazungumzo.

Tabora United, iliyomaliza nafasi ya tano msimu uliopita katika Ligi Kuu Tanzania Bara, inatarajia kutangaza wachezaji waliowasajili na kuwaacha wiki ijayo.

Kocha wao wa zamani, Anicet Kiazayidi, naye anahusishwa na kujiunga na Dodoma Jiji kuchukua nafasi ya Mecky Maxime.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *