Tanzania kuanza mapinduzi ya Cold Chain kwa mazao yanayoharibika haraka – Mkutano mkubwa kufanyika Dar

Mkutano huo utafanyika siku ya Jumatatu, tarehe 2 Juni 2025jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 1:00 jioni. Tukio hilo litawakutanisha viongozi wa juu wa serikali wakiwemo mawaziri kutoka wizara za KilimoBiasharaMifugo na Uvuvi, pamoja na Uchukuzi, sambamba na wadau kutoka sekta binafsi, mashirika ya maendeleo, wauzaji wa bidhaa nje ya nchi, watoa huduma za usafirishaji, na taasisi za kijamii.

Cold Chain: Suluhisho la Upotevu wa Mazao na Uboreshaji wa Ubora

Mpango wa kitaifa wa cold chain unalenga kuleta mageuzi makubwa katika uhifadhi na usafirishaji wa bidhaa zinazoharibika kwa haraka — kama matunda, mboga mboga, samaki, na nyama — kutoka mashambani hadi masoko ya ndani na ya nje. Kwa mujibu wa Vanguard Global Development, mpango huu utawezesha:

  • 📌Kupunguza kwa kiwango kikubwa upotevu wa mazao baada ya kuvuna
  • 📌Kutoa msaada wa moja kwa moja kwa wakulima wadogo, wavuvi na wafugaji zaidi ya 100,000 nchini
  • 📌Kuimarisha utoaji wa vyeti vya ubora na usalama wa bidhaa, hatua muhimu kwa bidhaa za kuuza nje
  • 📌Kujenga mtandao wa kisasa wa usafirishaji kwa kutumia teknolojia ya uhifadhi wa baridi, kupitia ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi (PPP)

Akizungumzia tukio hilo, Mujwahuzi Alexander, kutoka Vanguard Global Development alisema:

“Tunatamani kuiona Tanzania ikiimarisha mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo kwa kujenga miundombinu ya uhifadhi na usafirishaji wa baridi ambayo ni ya kuaminika na inayoendeshwa na teknolojia.”

Wadau wanaotamani kushiriki wanahimizwa kuwasiliana mapema kupitia:
 📧 Barua pepecontact@vanguardglobal-development.com
📞 Simu: +255 763 737 374

Mpango huo unatarajiwa kuwa kichocheo cha mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo, biashara ya bidhaa zinazoharibika, kuongeza ajira, na kuinua uchumi wa vijijini, huku ukilenga kuongeza mapato ya mauzo ya nje ya bidhaa bora kutoka Tanzania.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *