Tanzania kushiriki Kabaddi Malaysia

Tanzania itashiriki mashindano ya Dunia ya Kabaddi ya ufukweni yatakayofanyika Malaysia kuanzia Septemba 23–29 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Chama cha Kabaddi Tanzania, Abdallah Nyoni alisema timu za wanaume na wanawake zitaiwakilisha nchi na zitaingia kambini Septemba 8 jijini Dar es Salaam.

Alisema lengo ni kufanya vizuri na kuitangaza Tanzania kimataifa huku akitoa wito kwa wadau kusaidia vifaa na posho kwa wachezaji.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *