Friday, December 12, 2025
spot_img
HomeBiasharaTanzania na Oman Kuimarisha Ushirikiano wa Biashara

Tanzania na Oman Kuimarisha Ushirikiano wa Biashara

Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) wamekutana na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Oman jijini Dar es Salaam, wakijadili fursa za uwekezaji kwenye sekta muhimu ikiwemo kilimo, viwanda, mafuta na gesi, uchumi wa buluu, nishati mbadala, mifugo na uvuvi.

Rais wa TPSF, Angelina Ngalula, alisema mkutano huu ni matokeo ya ziara ya Rais Samia nchini Oman na ni fursa ya kuongeza thamani kwenye uchumi wa Tanzania. Pia alitangaza mpango wa kupeleka wafanyabiashara wa Tanzania Oman ili kuangalia fursa za soko.

Kiongozi wa ujumbe wa Oman, Dkt. Salem Al-Junaibi, aliahidi kuimarisha biashara ya pande mbili, huku Katibu Mtendaji wa TNBC, Dkt. Godwell Wanga, akisisitiza umuhimu wa kuboresha mazingira ya uwekezaji.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah, alisema Serikali imefanya mageuzi makubwa kuvutia wawekezaji na kufafanua kuwa biashara kati ya Tanzania na Oman imepanda kutoka Dola milioni 18 mwaka 2017 hadi zaidi ya Dola milioni 245 mwaka 2024.

Bidhaa zinazouzwa Oman kutoka Tanzania ni pamoja na nyama ya mbuzi, kaa, kahawa, maharage na juisi, huku bidhaa kutoka Oman zikiwa mafuta ya petroli, mbolea, saruji na vifaa vya umeme.

Sekta za kilimo hasa mafuta ya kula, ngano na mbogamboga pia zimetajwa kuwa na fursa kubwa za uwekezaji. Dkt. Al-Junaibi alihitimisha kwa kusema kuwa Tanzania na Oman zipo tayari kusaini mikataba ya kibiashara kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments