Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Suzan Kaganda, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika na Asia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Biashara za Kimataifa ya Zimbabwe, Mqabuko Dube.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Zimbabwe, viongozi hao walijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zimbabwe, hususan katika kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia pamoja na ushirikiano wa kikanda.
Aidha, pande zote mbili zilikubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo mbili na kushirikiana kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao.
Lengo la ushirikiano huo ni kuchochea maendeleo ya pamoja na kuimarisha zaidi uhusiano wa kirafiki uliopo kati ya Tanzania na Zimbabwe.





