
Chama cha ACT Wazalendo kimetoa wito kwa watanzania kuungana kuilazimisha Serikali kutekeleza wajibu wake katika kushughulikia tatizo la ajira nchini na kuhakikisha Serikali inaondoa mazingira kandamizi kwa watu wanaofanya shughuli zao za kujipatia kipato.
Aidha, chama kimewataka vijana na wazazi kutumia uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu ujao 2025 kuiangusha CCM kwa kushindwa kutatua tatizo la ajira.
Wito huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti Bara Isihaka Mchinjita akiwa jimboni Mlimba, Mkoani Morgoro Septemba 30, 2024 kutokana na ongezeko kubwa la vijana wanaohitimu ngazi mbalimbali za elimu kukosa ajira licha ya taifa kutumia gharama kubwa kuwasomesha.
“Mwaka huu peke yake [2024/25] fedha zinazotokana na kodi zenu takribani shilingi bilioni 800 zitatumika kusomesha watoto vyuo vikuu. Fedha hizi zitatolewa kama mikopo kwa wanafunzi ni kodi zenu mnazotozwa kwenye mazao huku, zingine mnaponunua bidhaa mnakatwa VAT. Tunafanya haya kila mwaka lakini ajira zinazozalishwa ni chache mnoâ€
Aidha, katika kutoonesha mwenendo wa tatizo la ajira, Makamu Mwenyekiti Bara Ndg. Isihaka Mchinjita amesema Serikali imeangusha uchumi na haijiangaishi kushughulikia tatizo la ajira licha ya kuwepo kwa mahitaji makubwa ya watumishi katika sekta ya elimu na afya.
“Kila mwaka vijana milioni moja wanaingia kwenye soko la ajira, uwezo wa Serikali ya CCM ya kuajiri kwa sasa ni vijana elfu 70 tu kwa mwaka kwahiyo kila mwaka vijana 930,000 wanarudi mtaani wakiwa hawana ajira. Imefikia mahali Serikali haijui kesho [future] ya kizazi cha Taifa hili.†Amesema Mchinjita.
Akifafanua upungufu wa watumishi amesema sekta ya elimu kuna upungufu wa walimu 279,202 na watumishi wa afya 121, 998. Lakini serikali haijaweka mkazo kuhakikisha sekta hizo zinapata wahudumu na wafanyakazi, licha ya kuwepo kwa vijana waliosomeshwa kwa gharama kubwa, serikali ina waacha mtaani wanakuwa machinga, bodaboda na mamantilie.

Kwa upande mwingine, Ado Shaibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo amesema mikopo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu inaliwa na wachache bila kuwanufaisha walengwa. Pia, kuwepo kwa changamoto ya upendeleo katika utolewaji wake na baadhi ya Halmashauri kutotenga kabisa.
“Sera ya serikali inasema 10% za mapato ya Halmashauri zisiguswe wapewe vijana, Wanawake na watu wenye ulemavu. Fedha hizi zinaliwa na wajanja wachache, Mkurugenzi anashirikiana na madiwani wanaunda vikundi hewa wanakopeshana wenyewe, wanakopeshana kiitikadi.â€
Ameongeza kuwa “maeneo mengi ya kanda ya ziwa niliyoenda nimekuta fedha hizi zinaliwa na wajanja wachache. Akina mama ambao walistahili kupata mikopo hawapati. Haya sio maneno yangu ni ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.†Ado Shaibu
Vile vile, ameeleza kuwa licha ya mchango wa sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji kwenye ajira lakini bado kilimo chetu hakijawekewa mkazo na serikali (bei isiyoeleweka, ruzuku hakuna na vivutio vya kikodi), hivyo kukifanya kilimo kuwa mzigo kwa nguvu ya vijana.
Viongozi wa Chama wanaendelea na ziara ili kuwafikia na kusajili wanachama milioni 10 kwa miezi 10 na maandalizi kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vijiji. Leo Makamu Mwenyekiti Bara atakuwa na Mkutano wa hadhara jimbo la Malinyi (Morogoro) na Katibu Mkuu atakuwa katika Jimbo la Karagwe (Kagera)