Kamati ya Uchaguzi ya TOC imetangaza wagombea waliopita mchujo wa awali wa nafasi mbalimbali za uongozi.

Tanzania Bara, waliopita ni pamoja na Henry Tandau na Leonard Katunzi (urais), na wajumbe kadhaa akiwemo Devota Marwa na Donald Masawe.
Kutoka Zanzibar, waliopita ni pamoja na Nassra Juma Mohamed (urais) na Suleiman Jabir (umakamu wa rais).
Mapingamizi yapokelewa leo na kesho, huku maamuzi yakitarajiwa kutolewa Septemba 16 kabla ya uchaguzi mkuu Oktoba 4, Morogoro.




