Sunday, April 5, 2026
spot_img
HomeHabariTraoré ahoji mfumo wa demokrasia

Traoré ahoji mfumo wa demokrasia

Rais wa mpito wa Burkina Faso, Ibrahim Traoré, amewaambia wananchi wa taifa hilo kuwa wanapaswa kusahau kuhusu demokrasia, akidai kuwa mfumo huo hauendani na mahitaji ya nchi yao.

Akizungumza katika mahojiano yaliyorushwa na televisheni ya taifa ya RTB, Traoré alieleza kuwa msingi wa demokrasia haujalengwa kwa ajili ya Burkina Faso, hivyo wananchi wanapaswa kuachana na dhana hiyo.

Kauli hiyo imezua mjadala mkubwa, ikizingatiwa kuwa Traoré aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi Septemba 2022 baada ya kuiondoa serikali nyingine ya kijeshi, na tangu wakati huo amekuwa akizuia sauti za upinzani.

Katika hatua nyingine, serikali ya kijeshi ilivunja tume ya uchaguzi mwaka jana na baadaye Bunge linaloongozwa na wanajeshi kupiga marufuku vyama vya siasa, ambavyo shughuli zake zilikuwa zimesimamishwa tangu mwaka 2022.

Hata hivyo, United Nations imeitaka Burkina Faso kubatilisha uamuzi huo na kusitisha ukandamizaji wa kisiasa, ikisisitiza umuhimu wa kuheshimu misingi ya demokrasia na haki za binadamu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments