Tundu Lissu alinyimwa ukumbi Makao Makuu Chadema?

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, amenyimwa Ukumbi wa kufanyia mkutano wake Makao Makuu ya Chadema kutokana na mgogoro wa kuwania uenyekiti ndani ya chama hicho na kulazimika kutangaza nia yake ya kuwania nafasi ya Uenyekiti katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Uamuzi wa Lissu wa kufanyia mkutano wake Mlimani City ulikuja saa chache baada ya kunyimwa ukumbi ndani ya Makao Makuu ya chama chao, hali inayoendeleza joto la mgogoro Chadema.

“Kwa jinsi tu minyukano jinsi ilivyo katika mitandao huko, tungefanyia Makao Makuu ingeweza kuleta sintofahamu. Tumekuja huku ili niwe na uwezo na uhuru wa kuzungumza na nyie wote bila hofu.

“Miezi michache iliyopita kuna bwana mmoja alitangaza nia ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa chama chetu na kama sikosei alitangazia nia hotelini pamoja na kwamba yeye ni Mwenyekiti wa Kanda ya Victoria,”Tundu Lissu Mgombea Uenyekiti Chadema.

Mgogoro wa Chadema unatokana na uwepo wa kambi mbili zinazomuhusisha Mwenyekiti wake Freeman Mbowe na Lissu wakichuana kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *