Twiga Stars kusuka au kunyoa leo dhidi ya Afrika Kusini

Twiga Stars, timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, leo inacheza mchezo wake wa pili wa Kundi C dhidi ya vinara Afrika Kusini katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON), mchezo wa kuamua hatma yao. Wanahitaji ushindi ili kubaki kwenye mashindano.

Kocha Bakari Shime amesema mchezo huu ni wa kuamua na wamejiandaa kwa tahadhari kubwa, akisisitiza kuwa ushindi utawapa matumaini ya kusonga mbele, huku akiongeza kuwa kurejea kwa mshambuliaji Opah Clement aliyekuwa na adhabu ya kadi tatu za njano ni faida kubwa kwa kikosi chake.

Mchezo huo utafanyika saa 4:00 usiku Uwanja wa Honneur, Oujda, Morocco. Twiga Stars walifungwa 1-0 na Mali kwenye mchezo wa kwanza, huku wakikosa baadhi ya wachezaji muhimu kwa sababu ya majeraha na adhabu.

Hadi sasa, Afrika Kusini na Mali zina pointi tatu kila moja, Tanzania na Ghana bado hazijapata pointi. Baada ya leo, Twiga Stars watamaliza hatua ya makundi dhidi ya Ghana Jumatatu ijayo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *