Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewataka mameneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuogeza spidi katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara.

Ulega amewaambia mameneja hao kuwa wanatakiwa waende kwa spidi inayofanana na viwango vya kasi vinavyoonekana wakati Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapopewa majukumu ya utekelezaji na serikali kwa sababu kuna mvua zinakuja na zinaweza kufanya maeneo yaliyoharibika kuharibika zaidi.
Ulega amesema barabara zilizoharibika kwa sababu ya mvua za masika zilizochanganyika na zile za El Nino zimesababisha usumbufu na kusimamisha shughuli za uchumi na hivyo ni muhimu zikashughulikiwa kwa haraka.