Monday, December 15, 2025
spot_img
HomeHabariUN: Tanzania kielelezo cha amani Duniani

UN: Tanzania kielelezo cha amani Duniani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema Tanzania imeendelea kuwa kielelezo cha amani na mshikamano wa kijamii barani Afrika na duniani, akisisitiza kuwa dunia inalitazama Taifa hilo kama mfano wa kuigwa.

Guterres ameyasema hayo leo, Desemba 14 Desemba 2025, alipokuwa akipokea ujumbe maalumu wa Tanzania uliotoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Kombo.

Katika maelezo yake, Guterres amegusia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu akisema, ulikuwa jaribio kubwa kwa taswira ya amani ya Tanzania, lakini taifa limevuka jaribio hilo, licha ya changamoto zilizojitokeza.

“Tungependa kuona Tanzania ikiendelea kuwa taifa lililoungana na mfano bora wa amani,” amesema Guterres.

Katibu Mkuu huyo wa UN amesisitiza umuhimu wa mazungumzo ya kitaifa jumuishi na yenye maana, ili kushughulikia chanzo cha matukio ya vurugu yaliyotokea wakati wa uchaguzi na kuzuia yasijirudie.

Pia ameahidi msaada wa Umoja wa Mataifa kwa Tanzania, hususan wakati na baada ya Tume ya Uchunguzi iliyoundwa na Serikali kukamilisha majukumu yake.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments