Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeHabariUwaziri Mkuu ni nafasi ya kuwatumikia Watanzania- Dk Samia

Uwaziri Mkuu ni nafasi ya kuwatumikia Watanzania- Dk Samia

Rais Samia Suluhu Hassan amesema nafasi ya uwaziri mkuu haihitaji urafiki, undugu na jamaa, badala yake ni nafasi ya kulitumikia Taifa.

Katika maelezo yake hayo, amemwambia Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba, kwa umri alionao wadhifa huo ni mzigo mkubwa kwake, kwani atakumbwa na vishawishi vya ndugu, jamaa na marafiki.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo, Ijumaa Novemba 14, 2025 alipohutubia baada ya uapisho wa Waziri Mkuu, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

“Tukutakie kazi njema, mzigo huu si mdogo na kwa umri wako, sijui Kassim aliingia akiwa na umri gani, mzigo huu ni mkubwa, kwa umri wako vishawishi ni vingi vya marafiki, ndugu, jamaa na wengine. Nafasi yako ile haina rafiki, ndugu wala jamaa ni nafasi ya kulitumikia Taifa hili,” amesema.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments