Uzalishaji maji waongezeka kwa 7%

Taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa mwaka 2023/2024 iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imeonesha ongezeko kubwa katika uzalishaji na usambazaji wa huduma ya maji nchini.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uzalishaji wa maji umeongezeka hadi kufikia mita za ujazo milioni 685, sawa na ongezeko la asilimia 7. Aidha, uwezo wa miundombinu ya uzalishaji wa maji umeongezeka kwa mita za ujazo milioni 51, ikiwa ni ongezeko la asilimia 72.

Vilevile, maunganisho ya huduma za maji yameongezeka kwa asilimia 9, kutoka kaya 1,532,362 mwaka 2022/2023 hadi kaya 1,669,298 mwaka 2023/2024, hatua inayodhihirisha maendeleo katika upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kwa wananchi.

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), alieleza mafanikio hayo wakati akiwasilisha bungeni mapendekezo ya bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2025/2026, katika kikao kilichoanza Mei 8, 2025.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *