Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi ya Wilaya ya Kongwa na wa nje ya Wilaya ya Kongwa wameshiriki ibada ya kuombea na kuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Job Ndugai katika Kanisa la Anglikana- Mtakatifu Machael, Dinari ya Kongwa Wilayani Kongwa leo Agosti, 11, 2025.





Ibada hii inaongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dk. Maimbo Mndolwa.









