Viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimkoa wamewasili katika viwanja vya Bunge, Jijini Dodoma, leo tarehe 10 Agosti 2025, kushiriki ibada maalum ya kuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Job Yustino Ndugai.

Ibada hiyo inaongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye anatarajiwa kuungana na Watanzania katika kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi huyo aliyelitumikia taifa kwa muda mrefu.











