Dirisha la usajili Ligi Kuu limechochea mvutano wa kuvutana wachezaji, hasa miongoni mwa timu za daraja la kati.

KMC imemsajili beki wa kati wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ibrahim Nindi, kutoka Mashujaa FC.
Wakati huo huo, JKT Tanzania imemchukua beki Paschal Mussa kutoka Mashujaa na Laurian Makame kutoka Fountain Gate, ambaye aliwahi kuvutiwa na Yanga.
Mbeya City nayo imemsajili mshambuliaji Habib Kyombo kutoka Singida Black Stars, akichukua nafasi ya Mudathir Said aliyejiunga na Mashujaa FC. Kyombo amewahi pia kucheza Simba, Fountain Gate (zamani Singida Big Stars) na Pamba Jiji.