Thursday, December 11, 2025
spot_img
HomeBiasharaWadau Nyanda za Juu Kusini wahamasishwa kushiriki Serengeti Awards 2025

Wadau Nyanda za Juu Kusini wahamasishwa kushiriki Serengeti Awards 2025

Wadau wa uhifadhi na utalii katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wamehamasishwa kushiriki katika Tuzo za Uhifadhi na Utalii za Serengeti (Serengeti Awards 2025) zinazotarajiwa kufanyika mwezi Desemba 2025.

Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii, Dainess Kunzugala, katika kikao na wadau wa sekta hiyo kilichofanyika Novemba 17, 2025 mkoani Iringa, kilichohusisha makampuni ya utalii, waongoza watalii, watoa huduma za malazi, wahifadhi pamoja na taasisi zinazochangia uhifadhi nchini.

Bi. Kunzugala amesema tuzo hizo zina kategoria saba zinazolenga kutambua na kuthamini mchango wa wadau katika kukuza uhifadhi na utalii, huku akisisitiza umuhimu wa washiriki kutumia fursa hiyo kujitangaza na kuongeza hamasa ndani ya sekta.

Amesema malengo makuu ni kuongeza mwamko katika utalii, kutambua juhudi za wadau na kuendelea kuifanya sekta hiyo kuwa nguzo muhimu ya maendeleo ya uchumi nchini.

Kwa upande wake, Bw. Fadhili Laizer, mwongoza watalii kutoka Mukuta Travel and Tours, ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kutoa elimu kuhusu namna ya kujisajili na kushiriki tuzo hizo, akiwataka wadau kujitokeza kwa wingi ili kukuza utalii na kuongeza mwonekano wa biashara zao.

Naye Mwenyekiti wa Iringa Tourism Association, Serafina Lanz, ameishauri Serikali kuangalia uwezekano wa kuziendeleza zaidi hifadhi za Nyanda za Juu Kusini kama Nyerere na Ruaha, na kupendekeza kuwa tuzo zijazo ziitwe kwa majina ya hifadhi hizo, kama Nyerere Awards au Ruaha Awards.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments