Wakaguzi kata za kisangura na Stand Kuu Serengeti Mkoa wa Mara Genuine Kimario na Nashoni Mchopa licha ya kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuchukia uhalifu na kutoa taarifa za wahalifu wameendelea pia kuangalia upande mwingine wa changamoto za wananchi wanao wahudumia ambapo wametoa kiti mwendo kwa kushirikiana na wananchi wenye mapenzi mema kwa mwananchi mwenye changamoto ya miguu.

Wakaguzi hao kwa pamoja wamebainisha kuwa licha ya jukum lao la msingi kuwalinda na raia na mali zao wanayonafasi ya kushirikiana na jamii katika kuwasaidia wananchi wenye changamoto mbalimbali katika Jamii.
Aidha wamewaomba wananchi kutambua kuwa wanakwenda katika kipindi cha uchaguzi wahakikishe wanaendelea kudumisha amani na kukataa kutumika vibaya na watu wenye nia ya kuchafua hali ya utulivu na amani.












