Tuesday, December 16, 2025
spot_img
HomeHabariWashiriki mafunzo waibua utalii wa Tanzania Kimataifa

Washiriki mafunzo waibua utalii wa Tanzania Kimataifa

Washiriki wa mafunzo ya Shirikisho la Polisi wa Wanawake duniani na wasimamizi wa sheria kutoka nchini Tanzania wameendelea kutumia vyema mafunzo wanayoshiriki nchini Scotland kutangaza uzuri na vivutio vilivyopo nchini Tanzania huku wakiwaomba washiriki hao kutoka mataifa zaidi ya 64 duniani wanaoendelea na mafunzo hayo kupanga kutembelea vivutio vilivyopo Tanzania.

Akiongea Baada ya kukutana na washiriki mbalimbali katika mafunzo hayo Mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP Julieth Lyimo kutoka nchi Tanzania akabainisha namna ambavyo wamewaalika washiriki kutoka mataifa mbalimbali duniani kufika na kuona maajabu ya dunia yaliyopo nchini Tanzania.

Ameongeza kuwa upekee wa Tanzania ni kuwa na vivutio vizuri na mtaji wa amani na utulivu wa nchi kitendo kinachoifanya Tanzania kuwa sehemu sahihi ya watalii kufurahioa maisha huku akiwaomba pindi wapatapo muda wa mapumziko wafike Tanzania kufurahi na kupumzika maeneo tofauti tofauti.

Kwa upande wa Mkaguzi wa uhamiaji Vashty Nyembera yeye akajinadi namna ambavyo Idara yake tayari imeweka mazingira rafiki kwa watalii wanaofika nchini Tanzania kwa ajili ya mapumziko na utalii kuwa wafike kwa wingi kutokana na maboresho ya viza kwa watalii kurahisishwa.

Mrakibu Msaidizi wa uhamiaji Siwema Lufeza akabainisha kuwa utalii wa Tanzania ni utalii wa tofauti na mataifa mengine huku akisisitiza kuwa wageni wengi na washiriki wa amafunzo hayo wameeleza namna ya filamu ya The Royal Tour ilivyo wasaidia kuifahamu Tanzania.
Koplo wa Jeshi la Polisi kutoka nchini Tanzania Venicia Paul yeye akaweka wazi kuwa licha ya kuwaomba kufika Tanzania kuona vivutio vilivyo na upekee wa nchi hiyo akabainsha kuwa yapo makabila na tamadunia nzuri ya kufurahia upekee wa Tanzania.

Vilevile Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Edina kadogo akasema kutokana na shughuli za utalii nchini Tanzania akasisitiza kwa wageni kuwa lipo dawati maalum la utalii katika Mkoa wa Arusha ambalo linatoa huduma bora za utalii na wanadiplomasia wanaofika nchini.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments