Wabunifu wa Kitanzania wamezindua jukwaa jipya la kidijitali la Piku, lenye mfumo wa mnada wa kipekee unaompa ushindi mshiriki aliyeweka dau dogo la kipekee lisilorudiwa na mwingine.

Piku, iliyosajiliwa rasmi na kupata leseni ya Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), inalenga kutoa zawadi mbalimbali za thamani kubwa kwa gharama ndogo.
Meneja Uendeshaji wa Biashara, Sia Malewas, amesema lengo ni kuleta ubunifu unaochangamsha akili na kuongeza msisimko wa kushinda zawadi.
Meneja wa Habari, Barnabas Mbunda, amesema washindi hupatikana kila wiki, mwezi na baada ya miezi mitatu, huku mshindi wa kwanza, Sabri Hamis kutoka Zanzibar, akijishindia vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni tano.
Mkaguzi kutoka GBT, Lucy Katamba, amesema jukwaa hilo limeendeshwa kwa uwazi na limeonesha mchango wa sekta ya michezo katika kukuza uchumi.

