Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeMichezoWatoto wa Mama Samia waiheshimisha Bendera ya Tanzania Kimataifa

Watoto wa Mama Samia waiheshimisha Bendera ya Tanzania Kimataifa

BONDIA Mtanzania Said Chino anaungana na Mabondia wengine wa Tanzania kwa kuweza kuipeperusha Bendera ya Tanzania kwenye pambano la kutetea mkanda wa International Boxing Association Inter-continental lightweight championship (IBA Inter-continental) baada ya kumpasua Bondia kutoka Afrika Kusini Malcolm Klassen kwa pointi za majaji wote watatu.

Chino amshinda pambano hilo la Raundi 10 lililopigwa usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Super Dome Masaki, ambapo Jaji namba moja ametoa pointi 99 kwa 91 Jaji namba mbili ametoa pointi 100 kwa 90 na Jaji namba tatu ametoa pointi 99 kwa 91.

Kwa ushindi huo, Said Chino ameubakisha mkanda wake wa IBA Tanzania na anaondoka na #KnockoutYaMama ya shilingi milioni tano kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

KnockoutYaMama

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments