Watu 11 wafariki dunia katika ajali mbaya Segera

Watu 11 wamepoteza maisha usiku wa kuamkia leo kufuatia ajali ya barabarani iliyosababishwa na lori lililokuwa limebeba saruji kupoteza mwelekeo na kuwagonga watu waliokuwa wamekusanyika kushuhudia ajali nyingine ya gari dogo aina ya Tata.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk. Batilda Buriani, ajali hiyo imetokea katika Kijiji cha Chang’ombe, Kata ya Segera, Wilaya ya Handeni.

Akizungumza na Nipashe tarehe 14 Januari 2025, Balozi Dk. Buriani alisema watu hao waliopoteza maisha walikuwa wamefika eneo la ajali hiyo kwa lengo la kutoa msaada na kushuhudia tukio, lakini kwa bahati mbaya wakakumbwa na ajali hiyo mbaya.

“Ajali hii imesababisha vifo vya watu 11 na kuacha wengine 11 wakiwa majeruhi. Tunatoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao na tunawaombea majeruhi wapone haraka,” alisema Dk. Buriani.

Viongozi wa eneo hilo wameendelea kutoa wito kwa wananchi kuwa waangalifu wanapokusanyika katika maeneo ya ajali ili kuepuka madhara kama hayo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *