Sunday, November 2, 2025
spot_img
HomeMichezoWavu Ufukweni: Tanzania yatua Burundi kutwaa Ubingwa wa Kanda

Wavu Ufukweni: Tanzania yatua Burundi kutwaa Ubingwa wa Kanda

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wavu Ufukweni imewasili salama mjini Bujumbura, Burundi, tayari kwa mashindano ya Kanda ya Tano yanayoanza leo hadi keshokutwa.

Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania (TVF), Shukuru Ally, alisema maandalizi yamekamilika na wachezaji wako kwenye hali nzuri kimwili na kiakili.
“Tumefanya mazoezi ya mwisho juzi kuhakikisha miili iko sawa. Tumejipanga kuhakikisha bendera ya Tanzania inapeperushwa vyema,” alisema Ally.

Timu hiyo inaundwa na wachezaji 8 — wanaume wanne na wanawake wanne — pamoja na makocha wawili na kiongozi mmoja.

Waliosafiri ni David Neeke (Kepler-Rwanda), Omary Bure (EAUR-Rwanda), Said Alhaji (KIUT), Selemani Hassan (Tanzania Prisons), Janeth Ajiri (JKT), Naima Mohamed, Evelyne Albert (Tanzania Prisons) na Mariam Omary (Star Girls), chini ya kocha Yusuph Mkalambati.

Ally alisema matumaini yao ni makubwa ya kurudi nyumbani wakiwa mabingwa.
“Kila mmoja anatambua wajibu wake. Tunajua Watanzania wanatarajia matokeo mazuri kutoka kwetu,” aliongeza.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments