Waziri Mkuu amwakilisha Rais Dk. Samia mazishi ya Hayati Job Ndugai

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Agosti 11, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Job Yustino Ndugai, yaliyofanyika shambani kwake, kijiji cha Msunjulile, wilayani Kongwa mkoani Dodoma.

Akizungumza katika ibada ya mazishi, Waziri Mkuu amewataka Watanzania kuenzi mema yote yaliyofanywa na marehemu Ndugai enzi za uhai wake, akisema mchango wake katika uongozi wa Bunge na Taifa kwa ujumla utabaki kuwa kumbukumbu muhimu kwa vizazi vijavyo.

amesema kuwa akiwa mwakilishi wa wananchi wa Kongwa, hayati Ndugai ametoa mchango mkubwa katika kipindi cha miaka 20 ya utumishi wake, na kwamba wote ni mashuhuda wa maendeleo makubwa yaliyopatikana katika sekta mbalimbali za maendeleo pamoja na huduma A kijamii. “Serikali tutaendelea kumuenzi kwa yale yote aliyoyafanya kwa wanaKongwa”

Aidha, Waziri Mkuu ameeleza kuwa marehemu alikuwa mlinzi wa taratibu za Bunge na mshirika wa karibu katika kuimarisha ushirikiano kati ya Bunge na Serikali kwa maslahi mapana ya Taifa, akisisitiza mawasiliano ya uwazi, mshikamano na mwelekeo wa pamoja katika utekelezaji wa ajenda za kitaifa.

Vilevile, Majaliwa amemtaja Ndugai kama kiongozi mwenye weledi, muadilifu, mnyenyekevu, na mchapakaI ambaye alibeba heshima ya mkoa wa Dodoma na jimbo la Kongwa kupitia uongozi na siasa za uwajibikaji.

Pia amesema kuwa Serikali itasiamia utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Rais Dkt. Samia ya kukamilishwa kwa masuala yote yaliyoanzishwa na Hayati Ndugai, pamoja na kuendeleza makumbusho ya Kongwa ikiwa ni kielelezo cha kupigania uhuru kwa nchi za kusini mwa afrika “Tusasimamia agizo hili kwa ukamilifu”

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, ametoa salamu za pole kwa familia ya marehemu, wananchi wa Kongwa na Watanzania wote kwa ujumla kutokana na msiba wa hayati Job Ndugai.

Hayati Job Ndugai alifariki agosti 06, 2025 jijini Dodoma kwa Shinikizo la damu lililoshuka sana.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *