
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry William Silaa, amezindua mradi wa maji na Zahanati yenye thamani ya sh.milioni 436.4 katika wilaya ya Mkalama, mkoani Singida.
1Mradi uliozinduliwa na Waziri Silaa ni zahanati ya Igonia iliyopo kijiji cha Mtogo Mwili uliogharimu sh. Milioni 87.4 ambao ulianza kutekelezwa kwa michango ya wananchi kabla ya serikali kumalizia ujenzi wake na itanufaisha wananchi 1,408 kulingana na sensa ya 2022.Â
Aidha, Mradi wa maji uliozinduliwa katika kijiji cha Nkalakala, umegharimu sh.milioni 348.9 na utapunguza changamoto kwa wananchi ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji.

Awali, Meneja wa RUWASA wilaya ya Mkalama, Mhandisi Christopher Saguda, alisema tanki la maji lililojengwa lina uwezo wa lita 90,000 litahudumia vituo 12 vya kuchotea na ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 100.
Katika hatua nyingine, Waziri Silaa amekagua mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi (VETA) katika kijiji cha Mwando, ambao umefikia asilimia 30 na unatarajiwa kugharimu sh. bilioni 1.4.

