Waziri Ulega atoa agizo kwa wakandarasi wa mradi wa mwendokasi

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewataka wakandarasi wanaosimamia ujenzi wa miundombinu ya mabasi ya mwendokasi jijini Dar es Salaam kuhakikisha wanakamilisha kazi kwa wakati kulingana na mikataba waliyoisaini.

Agizo hilo limetolewa Februari 5, 2025, wakati Waziri Ulega alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi hiyo, ambapo alionesha kusikitishwa na ucheleweshaji wa ujenzi kinyume na makubaliano ya awali.

Ameelekeza wakandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kufidia muda uliopotea, akisisitiza kuwa ucheleweshaji huo umeongeza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, Waziri Ulega pia amebaini changamoto za wafanyakazi wanaodai posho zao kwa muda mrefu pamoja na ukiukwaji wa mikataba yao ya ajira. Ametaka wakandarasi kuwaita waajiri wao haraka ili kushughulikia malalamiko hayo, akifafanua kuwa wafanyakazi hao hawaidai serikali bali makampuni husika.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule, ameahidi kufuatilia madai ya wafanyakazi hao ili kuhakikisha wanapata haki zao kwa mujibu wa mikataba yao ya ajira.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *