Tuesday, December 16, 2025
spot_img
HomeAfyaWizara ya Afya yapewa tuzo ya ushiriki bora katika Kongamano la MEL

Wizara ya Afya yapewa tuzo ya ushiriki bora katika Kongamano la MEL

Wizara ya Afya kupitia Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini imeibuka mshindi wa tuzo ya kuongoza kwa ushiriki mkubwa na kikamilifu katika Kongamano la Nne la Kitaifa la Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza (4th MEL Conference 2025), linaloendelea jijini Mwanza kuanzia Septemba 10 hadi 13, 2025.

Wizara ya Afya imetajwa kuwa ya kwanza kwa kupeleka washiriki wengi, wakiwemo wataalam wa kitengo cha ufuatiliaji na tathmini, wataalam kutoka idara na vitengo mbalimbali, miradi, hospitali za rufaa za mikoa, kanda na taifa, vyuo vya mafunzo ya afya ya kati, mabaraza na bodi za kitaaluma pamoja na taasisi zilizo chini yake kama MSD, NIMR, NHIF, TMDA na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Tuzo hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. James Kilabuko kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi, na kupokelewa na Bw. Kilwahila Kiiza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini.

Kongamano la MEL ni jukwaa muhimu la kitaifa linalojikita katika kubadilishana uzoefu, kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji na tathmini, pamoja na kujifunza mbinu bora za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments