
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso(Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Shirika la GIZ la Ujerumani kuhusu kuanzisha programu ya kuzinjegea uwezo watumishi na Taasisi za maji kuhusu masuala ya menejimenti na uongozi.
Mazungumzo hayo yaliyofanyika makao makuu ya GIZ, Eschborn nchini Ujerumani yanalenga kuendeleza mageuzi ya Sekta ya Maji nchini kuimarisha uwezo wa watumishi na uwezo wa Kitaasisi katika kusimamia na kutoa huduma za maji nchini kupitia kuandaa viongozi wa sasa na wajao wa Sekta.
Aidha, Waziri Aweso amesisitiza GIZ kuendelea kushirikiana na Wizara ya Maji katika kuwaandaa wataalamu katika utekelezaji wa Miradi mikubwa inayofadhiliwa na Taasisi za kifedha hususani za Ujerumani kama Benki ya Maendeleo ya Ujerumani KFW.


